Nyimbo za wokovu
Wimbo 15 Kutakuwa Na Baraka Maneno ya wimbo
Kutakuwa na baraka,
Hiyo ni Neno lake;
Kutakuwa na faraja,
Bwana hutoa kwake.
Baraka nyingi,
Baraka twahitaji;
Tumepokea kiasi,
Bali twataka nyingi.
Kutakuwa na baraka Ufufuo twataka;
Kwa mabonde na milima.
Mungu anyeshe mvua.
Kutakuwa na baraka,
zitumwagie Bwana:
Kurudishwa twataka,
Na mvua yako Bwana.
Kutakuwa na baraka,
Laiti zianguke;
Haja zetu twaungama,
Yesu, Utusikie.
Kutakuwa na baraka,
Tukimjua na kumtii;
Tena tutaburudishwa,
Tukimpa nafasi.