Nyimbo za wokovu
Wimbo 148 Yesu Ataka Kianga Maneno ya wimbo
Yesu ataka kianga,
Kung`ara daima;
Kwa Yesu niwe kianga,
Po pote daima.
Kianga, kianga,
Kwa Yesu niwe kianga;
Kianga, kianga,
Niwe kianga kwake.
Niwe mpenzi wa Yesu,
Niwapende wote;
Kuwaonyesha wengine Pendo siku zote.
Bwana Yesu, nimwulize
Anisaidie;
Moyo wangu utakaswe
Naye siku zote.
Niwe kianga kwa Yesu
Kuwa mwaminifu;
Nitumike naye Yesu,
Kisha nitamsifu.