Nyimbo za wokovu
Wimbo 14 Msifuni, Yesu Ndiye Mkombozi Maneno ya wimbo
Msifuni Yesu, ndiye Mkombozi;
Imbeni ya pendo zake kuu;
Sujuduni, malaika mlioko,
Jina lake liwe na sifa kuu.
Kama vile mchunga achungavyo
vivyo sisi kutwa atuchunga.
Msifuni mlio wake watoto
Msifuni aliye Mchunga.
Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi
Akateswa tupate ongoka;
Ndiye Mwamba, Dhamana ya kuokoka
Sujudini kwake Muangikwa,
Yesu aliyeudhiwa na hamu
Kwa pendo za Baba yake Mungu.
Alieyfyolewa na kusulubiwa,
Msifuni ndilo letu fungu.
Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi
Shindukeni, enyi malango, juu;
Bwana yesu tangu milele Mwokozi,
Mvikeni taji, ni yake tu.
Atukuja kuitawala nchi,
Yesu, Mwombezi wetu wa Mungu.
Msifuni, ni mfalme wa salama;
Ndiye kweli Mwana wake Mungu.