Nyimbo za wokovu
Wimbo 138 Mtazame Huyo Maneno ya wimbo
Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.
Mwenye-dhambi dhaifu, mtazame tu
Wala usifanye tashwishi.
Tazama! Tazama!
uishi!
Mtazame Huyo aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.
Kama siye Kondoo Mwondoa-dhambi,
Na makosa yako ya mumu!
Kama deni zetu zote hakulipa
Mbona imemwagika damu?
Si kutubu na sala ikomboayo
Ila damu ndiyo salama;
Ana aliyeimwaga aweza, sasa,
Dhambi zako kukufutia.
Usiwe na shaka, Mungu anasema,
Hakuna alilolisaza;
Hapo alipokuja alitimiza,
Kazi zote alizoanza.
Basi twae uzima kwa kufurahi
Upokee kwa Bwana, sasa,
Ujijue hakika kwake kuishi
Yesu, aishiye kabisa.