Nyimbo za wokovu
Wimbo 128 Mwokozi Ananiita Maneno ya wimbo
Mwokozi ananiita,
Mwokozi ananiita;
Mwokozi ananiita,
Nichukue msalaba wake.
Nitamwandama Mwokozi,
Nitamwandama Mwokozi;
Nitamwandama Mwokozi,
Nitakwenda naye daima.
Nitamfuata kazini,
Nitamfuata kazini;
Nitamfuata kazini,
Nitakwenda naye daima.
Nimfuate hukumuni,
Nimfuate hukumuni;
Nimfuate hukumuni,
Nitakwenda naye daima.
Atanipa utukufu,
Atanipa utukufu;
Atanipa utukufu,
Atakwenda nami daima.