Nyimbo za wokovu
Wimbo 11 Aitwa Wa Simanzi Maneno ya wimbo
Aitwa wa Simanzi,
Mwana wa mwenye enzi Mwenye mengi mapenzi!
Nasifiwe Bwana Yesu.
Akawa matesoni
Mungu Mwana yakini
Akatoka mbinguni
Nasifiwe Bwana Yesu.
Akapata dhihaka
Mzoe – mashaka
Ndiye yetu sadaka:
Nasifiwe Bwana Yesu.
Tu wenye dhambi sana,
Kwake dhambi hamna:
Na Mungu twapatana:
Nasifiwe Bwana Yesu.
Alikufa mtini
Akalia dhikini
Sasa yuko mbinguni:
Nasifiwe Bwana Yesu.
Punde atarejea
Yesu kutunyakua
Ndipo tutamwimbia,
Nasifiwe Bwana Yesu.