Nyimbo za wokovu
Wimbo 106 Nimekombolewa Na Yesu Maneno ya wimbo
Nimekombolewa na Yesu
Aliyenirehemi;
Kwa bei ya mauti yake Nimekuwa mtoto wake.
Kombolewa! Kombolewa!
Nakombolewa na damu;
Kombolewa! Kombolewa!
Mimi mwana wake kweli.
Kukombolewa na furahi,
Kupita Lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake,
Nimekuwa mtoto wake.
Nitamwona uzuri wake,
Mfalme wangu wa ajabu;
Nasasa najifurahisha
Katika neema yake.
Najua taji imewekwa
Mbinguni tayari kwangu;
Muda kitambo atakuja,
Ili alipo niwepo.