Nyimbo za wokovu
Wimbo 104 Ni Mwokozi Aliyenifia Maneno ya wimbo
Ni Mwokozi aliyenifia,
Nitoke dhambini, alisema,
Yeye aliyemwamini Mwana,
Anao uzima.
Amini, Amini, nakuambia,
Amini, Amini, ujumbe mpya;
Yeye aliyemwamini Mwana,
Anao uzima.
Dhambi zangu zilichukuliwa,
Deni zangu zote zililipwa;
Wote waliomwamini Mwana,
Wanao uzima.
Ijapo ningekuwa maskini,
Ijapo ningekuwa mkosaji;
Neno la furaha la Mwokozi,
Ninao uzima.
Na sina shaka, nitamwamini,
Yeye ajaye kwake hatupwi;
Amwaminiye, tuma habari.
Tunao uzima.