Nyimbo za wokovu
Wimbo 102 Neema Ya Mpendwa Bwana Maneno ya wimbo
Neema ya Mpendwa Bwana,
Neema ishindayo dhambi;
Pa Kalvari akamwaga damu,
Damu yake Mwana wa Mungu.
Ni neem, ni neema,
Neema iliyotakasa;
Ni neem, ni neema,
Neema ishindayo kosa.
Dhambi ni kama dhoruba kuu,
Iletayo hasara kwetu;
Bali Yesu ana neema,
Iuonyeshayo Msalaba.
Hatuwezi dhambi kuficha,
Tupateje kutuosha?
Tazameni damu ya Bwana,
Hiyo yafaa kutakasa.
Kweli neema ya ajabu
Yawajia waaminio;
Watakao kumwona Yesu,
Pokeeni neema hiyo.