Nyimbo Za Sifa
Wimbo 89 Siku ya Mbingu Kujawa na Sifa. Maneno ya wimbo
Siku ya Mbingu kujawa na sifa
Dhambi zilizidi duniani
Yesu akaja azaliwa mtu
Awe na watu ulimwenguni
Chorus
Alinipenda, alinifia
Ameondoa na dhambi zangu
Alifufuka nipewe haki
Yuaja tena Mwokozi wangu
Na siku moja walikwenda naye
Wakamkaza Msalabani
Aliumia, aliaibishwa
lli atuaokoe dhambini
Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini alipumzika
Matumaini yetu wenye dhambi
Ni Mwokozi, kwake twaokoka
Kaburi likashindwa kumshika
jiwe likatoka mlangoni
alifufuka kwa kushinda kwake
Naye yuko milele Mbinguni
Siku moja atatujia tena
Utukufu wake tutaona
Atawaleta na wapenzi wetu
Mwokozi wangu, tutaonana