Nyimbo Za Sifa
Wimbo 74 Msalabani pa Mwokozi. Maneno ya wimbo
Msalabani pa Mwokozi
Hapo niliomba upozi
Akaniokoa Mpenzi
Mwana wa Mungu
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu
Akaniokoa Mpenzi, Mwana wa Mungu
Chini ya Mti msumbufu
Niliomba utakatifu
Alinikomboa kwa damu
Mwana wa Mungu
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu
Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu
Aliniokoa dhambini
lkawa kunikaa ndani
Aliponifia Mtini
Mwana wa Mungu
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu
Aliponi?a Mtini, Mwana wa Mungu
Damu ya Yesu ya thamani
Huniokoa makosani
Huniendesha wokovuni
Mwana wa Mungu
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu
Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu
Hicho kijito cha gharama
Leo jivike kwa kuzama
Kwake uuone uzima
Mwana wa Mungu
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu
Kwake uuone uzima,Mwano wa Mungu