Nyimbo Za Sifa
Wimbo 54 Ni Siku Kuu Siku Ile. Maneno ya wimbo
Ni siku kuu siku ile
Ya kumkiri Mwokozi
Moyo umejaa tele
Kunyamaza hauwezi
Chorus
Siku kuu! siku kuu!
Ya kuoshwa: dhambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu
Ananiongoza miguu
Siku kuu, siku kuu!
Ya kioshwa dhambi zangu kuu
Tumekwisha kupatana
Mimi wake,Yeye wangu
Na sasa nitamwandama
Nikiri neno la. Mungu
Moyo tulia kwa Bwana
Kiini cha raha yako
Huna njia mbili tena
Yesu ndiye njia yako
Nadhiri yangu ya mbele
Nitaiweka daima
Hata ije siku He
Ya kwonana kwa salama