Nyimbo Za Sifa
Wimbo 53 Nipe Moyo Wenye Sifa. Maneno ya wimbo
Nipe moyo wenye sifa
Sio wa utumwa
Moyo ulionyunyizwa
Damu ya thamani
Moyo msikizi, moyo
Wa kunyenyekea
Moyo utawaliwao
Na Mwokozi pia
Wenye kutubu, mnyonge
Sadiki, amini
Kamwe, kamwe asitengwe
Akaaye ndani
Mpya, mwema na mawazo
Mwingi wa mapenzi
Nawe uwe kielelezo
Moyo wa Mwokozi
Ni uule moyo wako
Moyo wa huruma
Yesu, natamani kwako
Kukujua vyema
Na ya midomo matunda
Yako, nipe nami
Amani isiyokoma
Iwe yangu mimi
Nitie yako tabia
lnishukie juu
jina lako nipe pia
Ndilo la pendo tu
Ni wa Baba utuukufu
Mwana atukuke
Na Roho Mtakatifu
U Utatu pweke