Nyimbo Za Sifa
Wimbo 51 Wewe Umechoka Sana?. Maneno ya wimbo
Wewe umechoka sana?
Wataka raha?
Kwake Yesu utapata
Furaha
Alama anazo Yeye?
Sasa! makovu
Ya mikono, na miguu
Na mbavu
Nacho kimevikwa taji
Kichwa cha huba?
Alivikwa taji kweli
Miiba
Huku nikimfuata
Nipate nini?
Maonjo nje na ndani
Amani
Kwamba namwandama Bwana
Mwisho ni nini?
Ni furaha na salama
Mbinguni