Nyimbo Za Sifa
Wimbo 47 Nitwae Hivi Nilivyo. Maneno ya wimbo
Nitwae hivi nilivyo
Umemwaga damu yako
Nawe ulivyoniita
Bwana Yesu, naja, naja
Hivi nilivyo, si langu
Kujiosha roho yangu
Nisamehe dhambi zangu
Bwana Yesu, naja, naja
Hivi nilivyo, sioni
Kamwe furaha moyoni
Daima ni mashakani
Bwana Yesu, naja, naia
Hivi nilivyo, kipofu
Maskini na mpungufu
Wewe u mtimilifu
Bwana Yesu, naja, naja
Nawe hivi utanitwaa
Nisithubutu kukawa
Na wewe hutanikata
Bwana Yesu, naja, naja
Hivi nilivyo, mapenzi
Yamenipa njia wazi
Hali na mali sisazi
Bwana Yesu, naja, naja