Nyimbo Za Sifa
Wimbo 39 Yesu aIiniita,“Njoo”. Maneno ya wimbo
Yesu aIiniita,“Njoo,
Raha iko kwangu
Kichwa chako ukilaze
Kifuani mwangu
Nilikwenda kwake mara
Sana nilichoka
Nikapata kwake raha
Na furaha tena
Yesu aliniita,“Njoo,
Kwangu kuna maji
Maji ya uzima bure
Unywe uwe hai
Nilikwenda kwake mara
Na maji nikanywa
Naishi kwake, na kiu
Kamwe sina tena
Yesu aliniita,“Njoo,
Dunia ni giza
Ukinitazama nuru
Takung’arizia
Nilikwenda kwake mara
Yeye jua iangu
Ni kila wakati mwanga
Safarini mwangu