Nyimbo Za Sifa
Wimbo 32 Njoni! Wenye Dhambi. Maneno ya wimbo
Njoni! njoni! wenye dhambi
Njoni, msikawie
Yesu anawangojea
Ndiye awapendaye
Ajuaye awezaye
Kuwaponya ni Yeye
Ewe muhitaji uje
Anakukaribisha
lmani, kweli, na toba
Neema ya kutosha
jua sana, kwake Bwana
Bure utayapata
Njoni, mliolemewa
Na dhambi ya Adamu
Mkingoja kujiponya
Mtapotea mumu
Siwa haki, ni wakosa
Waoshwao kwa damu
Ikamtokea dhiki
Mle Gethisemani
Kisha alipoangikwa
Akalia Mtini
“lmekwisha,” alitosha
Dhabihu ya thamani
Kristo aliye Mbinguni
Hutuombea huko
Basi mtumai Yeye
Kamwe mwingine hako
Yesu pweke,Yesu pweke
Ndiye Mwokozi wako
Wamsifu _ sifu sana
Mbinguni malaika
Wachanganya nyimbo zao
Na waliookoka
Aleluya wataimba
Waliooshwa taka