Nyimbo Za Sifa
Wimbo 24 Yesu Unipendaye. Maneno ya wimbo
Yesu unipendaye
Kwako nakimbilia
Ni wewe utoshaye
Mwovu akinijia
Yafiche ubavuni
Mwako maisha yangu
Ni?kishe Mbinguni
Wokoe moyo wangu
Ngome nyingine sina
Nategemea kwako
Usinitupe Bwana
Nipe neema yako
Ninakuaminia
Mwenye kuniwezesha
Shari wanikingia
Vitani wanitosha
Nakutaka Mpaji
Vyote napata kwako
Niwapo muhitaji
Utanijaza vyako
Nao waangukao
Wanyonge wape nguvu
Poza wauguao
Uongoze vipofu
Bwana umeniosha
Moyo kwa damu yako
Neema ya kutosha
Yapatikana kwako
Kwako Bwana naona
Kisima cha uzima
Mwangu moyoni, Bwana
Bubujika daima