Nyimbo Za Sifa
Wimbo 2 Kale Nilitembea. Maneno ya wimbo
Kale nilitembea
Nikilemewa dhambi
Nilikosa Msaada
Kuniponya mateso
Chorus
Usi?we Msalaba!
Lisi?we kaburi!
Linalozidi yote
Asi?we Mwokozi!
Hata niliofika
Mahali pa Msalaba
Palinifaa sana
Sitasahau kamwe
Hicho ndicho chanzo
Cha kufurahi kwangu
Hapo ndipo mzigo
Uliponituliwa
Panapo Msalaba
Kinatolewa cheti
Cha kuingia Mbinguni
Kisicho cha kanisa
Yule bwana mjinga
Likwenda bila cheti
Kitumai kwingia
Kama walio nacho
Lipofika langoni
Akaulizwa cheti
Cha kumwonyesha Bwana
Akakutwa hanacho
Lituhuzunishalo
Ni ninyi msio nacho
Kuwa kama mjinga
Kwe. siku ya arusi!
Ubavuni mwa Yesu
Mlitokea damu
Chemchemi ya. uzima
itakasayo roho
jitahidi wingie
Damuni mwa Mwokozi
Utafutiwa dhambi
Toka rohoni mwako