Nyimbo Za Sifa
Wimbo 182 Tawaona tena hao Wapenzi. Maneno ya wimbo
Tawaona tena hao wapenzi
Waiiowasili mbele hapo
Tutaonana mapambaukoni
Nchi hiyo wapumzikapo
Nitawajua, wajapo ni wengi
Wacakaokutanika hapo
Sauti zao nitazitambua
Nchi hiyo wapumzikapo
Maisha yao yaliniongoza
Yalinifurahisha nilipo
Nitawaona huko kwenye raha
Nchi hiyo wapumzikapo
Sipendi warudi kutoka juu
Nitasubiri hata niwepo
jesu atanipa wapenzi wangu
Nchi hiyo wapumzikapo
Bwana jesu twongoze kwa mapenzi
Tu?ke nasi hapo walipo
Kwa rehema zako tutaonana
Nchi hiyo wapumzikapo