Nyimbo Za Sifa
Wimbo 170 Bwana Jesu,Twaungama. Maneno ya wimbo
Bwana jesu, twaungama
jina Iako sasa
Twashukuru kwa furaha
Kwani imepasa
Sana tumesharikana
Na waliokutii
Nao wakushuhudia
Kwa amri yako hii
Twaona ajabu kuu
Ya shauri lako
Una mapenzi makuu
Hekima ni yako
Twakumbuka dhiki yako
Kufa kwa taabu
Kujitia nafsi yako
Chini ya ghadhabu
Tena ulivyofufuka
Vyaonyesha vyema
Sisi tunafungamana
Na Wewe daima