Nyimbo Za Sifa
Wimbo 162 Lako Bwana, la Rehema. Maneno ya wimbo
Lako Bwana, la rehema
Nimesha Iishika
Ndiyo maagizo mema
Nitakukumbuka
Mwili kwa ajili yangu
Chini uliwekwa
Ukawa Mkate wangu
Nitakukumbuka
Damu yako ya thamani
Iliyomwagika
Kwa divai kikombeni
Nitaikumbuka
Siwezi kukusahau
Ulivyosumbuka
Maumivu, jasho, kiu
Nitakukumbuka
Msalaba wako kwangu
Kweli ni baraka
jesu, U Sadaka yangu
Nitakukumbuka
Na sasa natumaini
Niliyeokoka
Utakaporudi chini
Utanikumbuka