Nyimbo Za Sifa
Wimbo 158 Baba U Mwenye Mapenzi Makuu. Maneno ya wimbo
Baba U mwenye mapenzi makuu
Ulyetupa afe, mwanayo
Na sasa atuombeayo juu
Sisi twakujia saa hiyo
Twatimiza maagizo yake
Twakuomba kwa sadaka yake
Hatustahili kukujilia
Hata kuzoa makombo chini
Utuangalie twatubia
Ndiye Mkombozi na Kuhani
Kifuani mwake achukua
Majina yetu anatujua
Tusikize, sisi ndani yake
Tumenyunyiziwe hiyo damu
Toa nuru zako tung’ariwe
Tupe katika hii karamu
Kuonja utukufu wa mbingu
Na baraka yako Baba Mungu
Nasi Baba miguuni pako
Hatujiombei wenyewe tu
Wapenzi wetu kila waliko
Twawaombea, Mlinzi mkuu
Walinde, waongoze, washike
Wawe wako wasitukusike
Na Baba kabla hatujakwenda
Kwa vile ulivyotununua
Tu wako kabisa, twakupenda
Navyo vyote twakusongezea
Kwa myoyo ya kupenda tu wako
Hata utakapotwita kwako