Nyimbo Za Sifa
Wimbo 144 Mwokozi Wangu Mpendwa Nataka. Maneno ya wimbo
Mwokozi wangu mpendwa nataka
Niwe wako kabisa mwaka huu
Mawazo na vitendo, mambo yote
Yawe uyapendayo Wewe tu
Niwe wako Wewe, nitwae Bwana
Tengeza maisha upendavyo
Ninakupa nafsi yangu kabisa
Kwa mema na kwa mabaya vivyo
Nakupa moyo, sasa nikupende
Kuliko myaka yaliyopita
Nifanyayo yote yawe furaha
Siku zote nikupende sana
Nakupa nia, Bwana ikubali
Usiponishika nitaasi
Mimi siwezi neno, nitawale
Nili mikononi mwako, basi
Nipe Roho wako na kunituma
Niende hubiri neno lako
Jema, la kweli, lenye kuokoa
Wafufuke wafu, waje kwako