Nyimbo Za Sifa
Wimbo 134 Njioni na Furaha Enyi wa lmani. Maneno ya wimbo
Njoni na furaha, enyi wa imani
Njoni Bethilehemu upesi
Amezaliwa jumbe la Mbinguni
Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu
Njoni tumuabudu Mwokozi
Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga
Amekuwa radhi kuzaliwa
Mungu wa kweli, wala si kiumbe
Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu
Njoni tumuabudu Mwokozi
Jeshi la mbinguni, imbeni kwa nguvu
Mbingu zote na zijae sifa
Sifuni Mungu aliye mbinguni
Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu
Njoni tumuabudu Mwokozi
Ewe Bwana mwema, twakubarikia
Jesu, utukufu uwe wako
Neno la Baba limekuwa mwili
Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu
Njoni tumuabudu Mwokozi