Nyimbo Za Sifa
Wimbo 128 Yesu Mponya. Maneno ya wimbo
Yesu ndiye mganga wetu
Aponya wagonjwa wote
Mganga wetu niYesu
Aponyaye hasira
Chorus
Tumsifu huyo,Yesu
Tumsifu milele
Kwani Mponya mtakota
Mwokozi wa wanyonge
Mganga wetu ni Yesu
Huondoa matusi
Mganga wetu ni Yesu
Mwenye kuponya choyo
Mganga wetu ni Yesu
Huponya wivu wetu
Yesu ndiye aponyaye
Kelele za nyumbani
Mganga wetu ni Yesu
Mponya wa tamaa mbaya
Mganga wetu ni Yesu
Washerati hufuta
Mganga wetu ni Yesu
Aponya kiu cha pombe
Mganga wetu ni Yesu
Kila dhambi aponya.