Nyimbo Za Sifa
Wimbo 125 Juu Yake Langu Shaka. Maneno ya wimbo
Juu yake Iangu shaka,
Yesu namuwekea,
Nami sitafedheheka
Nikimtegemea,
Natumai, natumai,
Natumai kwake tu;
Natuman, natumai,
Natumai kwake tu.
Juu yake dhambi zangu;
Aniosha kwa damu;
Nionekane kwa Mungu
Nisiye na Iaumu.
Juu yake yangu hofu;
Kwake nimetulia;
Sipotei kwa upofu
Njia aning’azia.
Juu yake raha yangu;
Humuangalia tu;
Mwenye kila uiimwengu
Aniruzuku na huu.
Juu yake, moyo wangu;
Hali yangu na mali;
Mimi wake, Yeye wangu
Twapasana kamili.