Nyimbo Za Sifa
Wimbo 112 Enyi Wanadamu. Maneno ya wimbo
Enyi wanadamu mbona
Sana mwatanga-tanga,
Kama kondoo wanyonge,
Wasio na mchunga?
Yuko Mchunga Mmoja
Mwenye mapenzi mama;
Haya kutaneni kwake,
Atawachunga vyema.
Mungu tunamwona kuwa
Mwenye uwezo wote;
Na nguvu zake zapita
Mawazo yetu yote;
Ni Baba, mapenzi yake
Ni makubwa hakika;
Hatuwezi kuyajua
Na hayana mpaka.
Rehema za Mungu nazo
Zina upana sana;
Kama huo wa bahari,
Mwisho wake hapana;
Haki yake ina mema.
Kwa hayo twashukuru,
Kwetu uko msamaha
Furaha na uhuru.
Mapenzi yake mapana,
Slsi hatuna cheo
Cha kutosha, nao moyo
Una wema upeo;
Ukombozi mwingi mno
Katika damu yake;
Sote twapata furaha
Kwa maumivu yake.
Yesu mkaribieni
Njoni kwaka kwa imani,
Mama yake ni hayo
Heri tuwa kama wana
Tushike neno Iake.
Daima atatujaza
Tele furaha yake.