Nyimbo Za Sifa
Wimbo 105 Neno Lako, Bwana. Maneno ya wimbo
Neno lake Bwana
Ni imara sana
Lilo Iatwongoza
Lilo latufunza
Adui wabaya
Wakikaribia
Neno lake Bwana
Ni ulinzi sana
Siku za dhoruba
Soma ukiomba
Neno lake Bwana
Msaada sana
Ukiliamini
Hwenda na amani
Una na furaha
Neno ni silaha
Ni furaha kweli
Na wingi wa mali
Neno lake Bwana
Kwa wasiokana
Neno Ia rehema
Tukali wazima
Faraja i papo
Tufarikanapo
Tulijue sana
Neno lake, Bwana
Hapa tukupende
Kisha kwako twende