Nyimbo Za Sifa
Wimbo 103 Nitaimba ya Yesu. Maneno ya wimbo
Nitaimba ya Yesu
Kwa rehema zake
Baraka nyingi sana
Nimepata kwake
Nitaimba ya Yesu
Sadaka ya Mungu
Alimwaga damu
Ukombozi wangu
Nitaimba ya Yesu
Hapa siku zote
Nitakapokumbuka
Vyema vyake vyote
Nitaimba ya Yesu
Hata mashakani
Yeye atanilinda
Mwake ubavuni
Nitaimba ya Yesu
Niwapo njiani
Takaza mwendo, hata
Nifike Mbinguni
Nikiisha ingia
Mlangoni mle
Yesu nitamwimbia
Mbinguni milele