Nyimbo Za Sifa
Wimbo 102 Twenenda Sayuni. Maneno ya wimbo
Mpendao Bwana
Ije raha yenu!
lmbeni nyimbo za raha
Wa ibada yenu
Twenenda sayuni
Mji mzuri Sayuni
Twenenda juu Sayuni
Ni masikani ya Mungu
Wasiimbe wao
Wasioamini
Watoto wa Mungu ndio
Waimbao chini
Twaona rohoni
Baraka za Mungu
Tusijafika Mbinguni
Kwenye utukufu
Tutakupomwona
Masumbuko basi
Huwa maji ya uzima
Anasa halisi
Tupaaze sauti
Na fute machozi
Twenenda kwa lmanweli
Naye ni Mwokozi