Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 7 MUNGU MSAADA WETU nyimbo za wokovu
1
Mungu msaada wetu,
Tangu miaka yote,
Ndiwe tumaini letu,
La zamani zote.
2
Kivuli cha kiti chako,
Ndiyo ngome yetu,
Watosha mkono wako,
Ni ulinzi wetu.
3
Kwanza havijakuweko,
Nchi na milima,
Ndiwe Mungu chini yako,
Twakaa salama.
4
Na miaka elfu ni kama,
Siku moja kwako,
Utatulinda daima,
Tuwenyeji wako.
5
Bwana msaada wetu,
Tangu miaka yote,
Mlinzi wetu na ngome,
Daima milele.