Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 66 ROHO YANGU AMKA SASA nyimbo za wokovu
1
Roho yangu amka sasa,
mara jitahidi;
Shindano ni lake Bwana,
Zawadi ni taji.
2
Sauti ni yake Mungu
inayokuita;
Ndiye aliyekirimu
taji la uzima.
3
Mashahidi ndio wengi
wanaokuona;
Ya nyuma usifikiri
bali mwendo kaza.
4
Bwana umetuanzisha
katika shindano;
Kwa vile tunaposhinda
ushindi ni wako.