Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 63 NIUONAPO MSALABA nyimbo za wokovu
1
Niuonapo Msalaba,
Kristo aliponifia;
Kwangu pato ni hasara.
Kiburi nakichukia.
2
Na nisijivune, Bwana,
Ila kwa sadaka yako;
Upuzi sitaki tena,
Zi chini ya damu yako.
3
Tangu kichwa hata nyayo,
Zamwagwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo.
Pendo zako zimetimu.
4
Vitu vyote dunia,
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zaniwia,
Nafsi, mali, na maisha.