Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 62 NAPENDA KITABU CHAKE nyimbo za wokovu
1
Napenda kitabu, chake,
Kilichotoka mbinguni,
Barua kwangu ya Bwana
Ujumbe wake wa ‘pendo’.
2
Humo ndani ya kitabu
Sura ya Yesu naona;
Karatasi zimekuwa,
Wayo zake za Mwongozi.
3
Neno lake ni maonji,
Kubwe la asali tamu;
Natamani kuuonja,
Ule mkate wa uzima.
4
Mapenzi Yake Mwumbaji,
Yanafunuliwa humo;
Hazina kuu ya hekima,
Utajiri wa ajabu.
5
Mwangaza wa ulimwengu
Angaza humo moyoni!
Uwe mwandamizi pote,
Taa ya hatua zangu