Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 6 KUMEKUCHA KWA UZURI nyimbo za wokovu
1
Kumekucha kwa uzuri,
Nafumbua macho;
Baba amenihifadhi,
Ni wake mtoto.
2
Bwana niwe leo kutwa
Ulinzini mwako;
Nisamehe dhambi,
Niwe Mikononi mwako.
3
Roho wako anikae
Moyoni daima;
Anitakase, nione
Uso wako mwema.