Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 54 NATAKA NIMJUE YESU nyimbo za wokovu
1
Nataka nimjue Yesu,
na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake tu,
wokovu wake kamili.
Zaidi, zaidi,
nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake,
wokovu wake kamili.
2
Nataka nione Yesu,
na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni,
kujidhihirisha kwangu.
3
Nataka tena zaidi,
daima kupambanua
Mapenzi yake, nifanye
yale yanayompendeza.
4
Nataka nikae naye,
kwa mazungumzo matamu.
Nizidi kuwaonyesha
wengine wokovu wake.