Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 46 MIGUUNI PAKE YESU nyimbo za wokovu
1
Miguuni pake Yesu,
Maneno yake tamu;
Pahali palipo heri,
Niwepo kila siku.
Miguuni pake Yesu,
Nakumbuka upendo
Na hisani vyake kwangu,
Vimenivuta moyo.
2
Miguuni pake Yesu,
Hapa pahali bora
Pa kuweka dhambi zangu
Pahali pa pumziko
Miguuni pake Yesu,
Hapa nafanya sala
Kwake napewa uwezo,
Faraja na neema
3
Unibariki Mwokozi
Ni miguuni pako,
Unitazame kwa pendo,
Nione uso wako
Nipe Bwana nia yako
Ili nionekane
Nimekaa na Mwokozi
Aliye haki yangu