Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 39 ATI, KUNA MVUA NJEMA nyimbo za wokovu
1
Ati, kuna mvua njema
yanya yenye neema;
Watu wanaona vyema
Bwana huninyeshei?
Na mimi? Na mimi?
Bwana, huninyeshei?
2
Sinipite, Baba Mwema,
dhambini nimezama:
Rehema ni za daima:
Bwana, hunionyeshi?
3
Sinipite, Yesu Mwema,
Niwe nawe daima,
Natamani kukwandama:
Bwana, hunichukui?
4
Sinipite, Roho Mwema,
Mpaji wa uzima,
Nawe shahidi wa wema,
Bwana wema hunipi?