Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 38 NASIFU SHANI YA MUNGU nyimbo za wokovu
1
Nasifu Shani Ya Mungu,
mweneza bahari,
Muumba pia wa mbingu,
jua, nyota, mwezi,
Ni tukufu lako shani,
mtengeza mambo
Ya nyakati na zamani,
yasiyo na mwisho.
2
Kadiri ya nionayo,
ya kusifu Mungu:
Nchi niikanyagayo,
na hayo mawingu;
Hakuna hata unyasi,
usiokukuza;
Na upepo wavumisha,
au kutuliza.
3
Nami kwa mkono wako,
naongozwa sawa,
Ni pato nikusifupo,
kukwona ni dawa;
Umenizingira nyuma,
na mbele Baraka;
Maarifa ya ajabu!
Yanishinda mimi!