Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 3 MUNGU ATUKUZWE nyimbo za wokovu
1
Mungu atukuzwe
Kwa mambo makuu,
Upendo wake
Ulitupa Yesu,
Aliyejitoa
Maisha yake,
Tuwe nao
Uzima wa milele.
Msifu, Msifu,
Dunia sikia,
Msifu, Msifu,
Watu wafurahi,
Na uje kwa Baba
Kwa Yesu Mwana,
Ukamtukuze
Kwa mambo yote.
2
Wokovu kamili
Zawadi kwetu,
Ahadi ya Mungu
Kwa Ulimwengu,
Wanaomwamini
Na kuungama,
Mara moja
Wale husamehewa.
3
Alitufundisha
Mambo makuu,
Alihakikisha
Wokovu wetu,
Lakini zaidi
Ajabu kubwa,
Yesu atakuja
Na tutamwona.