Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 21 BABA TWAKUJIA nyimbo za wokovu
1
Baba twakujia,
Uwe msaada;
Uwe kimbilio,
Twakusihi.
Dunia ni giza
Tukitengwa nawe;
Tufariji hapa,
Baba yetu.
Baba twakujia,
Tu dhahifu,
Usitugeue,
Tusikie.
2
Salama tulinde,
Kati ya taabu;
Uwe raha yetu
Mashakani.
Roho yasumbuka,
Baba tujalie;
Twakuomba sana,
Tupe nguvu.
3
Neema utupe,
Tukubali kwako;
Moyo wetu linda,
Safarini;
Tuongoe mbele,
Tupate kushinda
Na Kufika ng’ambo,
Kule kwako.