Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 2 TWAMSIFU MUNGU nyimbo za wokovu
1
Twamsifu Mungu,
Mwana wa upendo,
Aliyetufia
Na kupaa juu,
Aleluya usifiwe,
Aleluya amen,
Aleluya usifiwe,
Utubariki.
2
Twamsifu Mungu,
Roho mtukufu,
Akatufunulia
Mwokozi wetu,
3
Twamsifu Mungu,
Aliyetufia,
Ametukomboa
Na kutuongoza,
4
Twamsifu Mungu,
Wa neema yote,
Aliyetwaa dhambi,
Akazifuta,
5
Tuamshe tena,
Tujaze na pendo,
Moyoni uwashe
Moto wake roho.