Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 199 UPENDO NI FURAHA nyimbo za wokovu
1
Upendo ni furaha,
Ni kweli desturi
Yake kuzisahihisha
Njia zetu zote.
Yu pendo:
Tu watoto wake.
Yu pendo,
Mwana wa Mungu!
Na sisi tupendane
Kama Baba Mungu
Amri yake ndiyo hii,
Kupendana sana.
2
Duniani huzuni,
Ugonjwa, mauti,
Kwa pendo tuwafariji
Wenye mahitaji.
3
Na atakapokuja
Kutuchukua juu,
Tutaimbia milele
Pendo lake Yesu.