Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 196 VITO VYA THAMANI nyimbo za wokovu
1
Kitambo Bwana yuaja
Atafute kote
Vito vya thamani kubwa;
Mali yake kuu
Kama nyota tajini
Vitang’aa sana.
Vito vizuri kweli
Vyenye thamani.
2
Karibu atakusanya
Vito kwa ufalme
Vizuri vinavyong’aa;
Mali yake kuu.
3
Watoto wote wadogo
Wampendao Yesu.
Ndiyo vito ving’aavyo;
Mali yake kuu.