Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 194 TWAOMBA BARAKA ZAKO nyimbo za wokovu
1
Twaomba, Bwana,
Umpokee Kama mhudumu;
Ambaye anajitoa
Kuwa mtumishi.
2
Twaomba, Bwana,
Umpokee Kama mhudumu;
Neno lako alitoe,
Mwangaza kung’aa.
3
Mwokozi wetu,
Twaomba, na umwandikie
Kitabuni mwako juu
Mjumbe wa injili.
4
Silaha zake apewe
Kumshinda adui;
Vitani awe hodari,
Mpaka mauti.
5
Yeye ashindaye, Bwana,
Kwa rehema yako,
Ile taji ya dhahabu,
Nawe utampa.