Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 185 MUNGU, MAPENZI MAKAMILIFU nyimbo za wokovu
1
Mungu u mapenzi mkamilifu
Yapitayo fahamu za watu
Twanyenyekea sisi wapungufu,
Wape Baraka wapenzi wetu.
2
Ewe Mapenzi yasiyopimika
Twawaombea kitini Mwako,
Wape mapenzi yasiyotindika,
Waliooana mbele yako.
3
Ewe uhai, wewe u dhamana
Ya imani na matumaini,
Wape kuvumilia hapa sana
Wasiche maumivu mwishoni.
4
Wape furaha hiyo iwezayo
Kutia nuru kwenye huzuni,
Wape amani hiyo itakwayo
Katika matata duniani.
5
Waende mbele kusaidiana
Maisha yao ulimwenguni;
Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu,
Wafurahi milele mbinguni.