Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 156 UNIONGOZE, YEHOVA nyimbo za wokovu
1
Huniongoze, Yehova,
Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, u hodari,
‘Nilinde kwa mkono.
Unitunze, unilinde,
Unionyeshe njia!
2
Na kisima cha uzima,
Maji ya utabibu,
Fungua kwa moyo wangu,
Ninywe na kuponyeka!
Uninyweshe, unilishe,
Hata nimetosheka.
3
Wakati wa kuuvuka,
Ule mto Yordani,
Hofu yangu ufariji,
‘Nione uso wako.
Nyimbo shangwe,
nyimbo shangwe,
Nitaimba daima.