Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 153 FIKIRA MOJA TU nyimbo za wokovu
1
Fikira moja tu
Hurejea tena;
Nimekaribia mbingu
Zaidi ya jana,
Karibu na Kwetu mbingu,
Karibu na kwetu sasa,
Nikwone karibu.
2
Karibu na kwetu
Na kwenye makao;
Kiti cha enzi cha Mungu,
Pahali pa mto.
3
Kamilisha, Yesu,
Kuamini kwangu;
Nikifika mwisho wangu,
Nikwone karibu.