Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 141 CHINI YA MSALABA nyimbo za wokovu
1
Chini ya msalaba
Nataka simama;
Ndio mwamba safarini,
Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu
Ni tuo kamili,
Tatua mizigo wangu
Wakati wa hari.
2
Hapa ni pema sana,
Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana,
Mapenzi ya Kweli;
Kama alivyoonyeshwa
Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa
Ngazi ya mbinguni.
3
Na Yesu msalabani
Walimkemea,
Alikufa niokoke
Niliyepotea,
Naona ajabu sana
Ya mambo mawili
Jinsi alivyonipenda
Nisiyestahili.
4
Atakayeonana
Na Yesu mbinguni,
Njia yake aanzapo
Ni msalabani;
Wokovu upo hapa tu,
Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu
Pamoja na Bwana.